Wednesday, May 13, 2015
Ticha ni jiniasi
Mwalimu aliingia darasani kwenye kipindi cha dini akiwa tafrani amechoka sana, akawambia wanafunzi wote wakae kimya, mara usingizi ukampitia akiwa palepale darasani, ghafla Mkaguzi akaingia akasimama pembenikwa yule mwalimu. Mara mwalimu alipozinduka toka usingizini huku akipiga miayo na kumuona mkaguzi akiwa pembeni yake, ndipo alipojibabaisha na kuwaambia wanafunzi "Na hivi ndivyo walivyolala wanafunzi wa YESU, walipokuwa wanamsubiri kule mlimani, Je kuna mwenye swali?" Mkaguzi akapiga makofi na kumsifia kwa kufundisha kwa vitendo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment