Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, wiki ijayo
atakamilisha uteuzi wa majina ya wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba,
uteuzi unaoashiria kuanza kwa bunge hilo litakalokuwa na wajumbe 640.
Bunge hilo litakaloanza mwanzoni mwa mwezi ujao
mjini Dodoma, litakuwa na kazi ya kuijadili na kuipitisha Rasimu ya
Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30 mwaka
jana.
Wajumbe wengine watakaounda Bunge hilo ni 42
kutoka vyama vya siasa, 358 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na 81 kutoka
Baraza la Wawakilishi.
Januari 2 mwaka huu, ilikuwa siku ya mwisho kwa
Ikulu kupokea majina ya makundi mbalimbali ya kijamii ambayo
yaliwasilisha mapendekezo ya majina ya watu ambao wangependa wawe
wajumbe wa Bunge hilo. Makundi zaidi ya 50 yaliwasilisha majina yao.
Makundi hayo ni asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya Serikali, vyama vya kitaaluma, madhehebu ya dini na vyama vya siasa.
Kuanza kwa Bunge hilo kunatarajiwa kuwa na mvutano
mkali kutokana na msimamo wa baadhi ya makundi hayo, hasa vyama vya
siasa ambavyo vimekuwa vikipingana zaidi katika mfumo wa Serikali tatu
uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
No comments:
Post a Comment