Wednesday, May 13, 2015
Fanya hivi
IFURAHIE leo ISAHAU jana USIFIKIRIE kuhusu kesho, kwasababu leo ni "ZAWADI" kesho ni "SIRI" kubwa na jana imebaki "HISTORIA"
Ni shiiida
Chizi kanunua gazeti kufika nyumbani kwao akaliweka kwenye Friji, Dada yake akamuuliza: "mbona gazeti umeliweka kwenye friji?" Chizi: Lina habari motomoto ngoja zipoe kwanza ndo nizisome.
Masematiki
Japo we ni bingwa wa hesabu amini nakuhakikishia (1 mara 3) sio sawa na (3 mara 1). Kama huamini nenda hospitali daktari akikuandikia (1mara3) wewe meza (3 mara1) uone kitacho kutokea.
Hasira hasara (HH)
Sikia hii: Mume na mke waligombana wakiwa safarini ndani ya gari lao. Ugomvi ulipozidi mume akapandwa na hasira akasema "wanawake wote ni mbwa tu" Mke akanyamazawakaendelea na safari wakaona mbwa anatembea kandokando ya barabara mke akasema :Mama yako yule anatembea.... simama tumpe lift" unataka kujua kilichoendelea ingia kwenye tovuti baada dakika kumi zijazo.
Ticha ni jiniasi
Mwalimu aliingia darasani kwenye kipindi cha dini akiwa tafrani amechoka sana, akawambia wanafunzi wote wakae kimya, mara usingizi ukampitia akiwa palepale darasani, ghafla Mkaguzi akaingia akasimama pembenikwa yule mwalimu. Mara mwalimu alipozinduka toka usingizini huku akipiga miayo na kumuona mkaguzi akiwa pembeni yake, ndipo alipojibabaisha na kuwaambia wanafunzi "Na hivi ndivyo walivyolala wanafunzi wa YESU, walipokuwa wanamsubiri kule mlimani, Je kuna mwenye swali?" Mkaguzi akapiga makofi na kumsifia kwa kufundisha kwa vitendo.
Ulevi nouma
Walevi wa3 walikodi Bajaji, Baada ya dereva kugundua kuwa wamelewa akaamua kufanya yake akaiwasha bajaji na kuipiga lesi za kutosha bila kuondoka kisha akaizima akawaambia wale jamaa(walevi) tumefika:
Wa1: Akashuka akamwambia asante.
Wa2: Akashuka akamlipa.
Wa3: Akampiga bonge la kofi na kumwambia siku nyingine usiendeshe kasihivyo.
SWALI: Yupi aliyekuwa kalewa kuliko wengine?!
Wa1: Akashuka akamwambia asante.
Wa2: Akashuka akamlipa.
Wa3: Akampiga bonge la kofi na kumwambia siku nyingine usiendeshe kasihivyo.
SWALI: Yupi aliyekuwa kalewa kuliko wengine?!
Subscribe to:
Posts (Atom)